KIPIMO CHA UJAUZITO (UPT)


  • Kipimo cha ujauzito hutumika kuthibitisha kama mwanamke ana ujauzito baada ya kuwa na dalili ambazo zinaashiria kuwepo kwa ujauzito, hiki kipimo hupima uwepo wa hormone ya HCG katika aidha mkojo au damu ya mama mjamzito, ambapo hii  hormone hutolewa mwilini pale tu mwanamke akiwa mjamzito takribani siku 6-10 baada ya mimba kutungwa.
  • Kama mwanamke hana ujauzito basi hormone ya HCG huwa haipatikani kwenye damu na mkojo wa mwanamke, lakini akiwa mjamzito hormone ya HCG hupatikana aidha kwenye mkojo au damu ya mama mjamzito.
  • Ukitaka kupima ujauzito mkojo au damu huchukuliwa; kwa njia ya mkojo, mkojo huchukuliwa na kuwekwa kwenye chombo safi, baadae kipimo huwekwa kwenye chombo chenye mkojo kwa muda wa sekunde 10-15 baadae hutolewa kwa kusoma majibu. Kupima ujauzito kwa njia ya damu, hii njia hufanyika maaabara tu. Kipimo huwa na mistari miwili ambapo kikichora mstari mmoja huashiria hakuna ujauzito na kikichora mistari miwili huashiria uwepo wa ujauzito.
                                         
  • Muda muafaka wa kutumia hiki kipimo ni pale tu mwanamke anapogundua kuwa amekosa damu zake za mwezi na ni vizuri kupima mapema au wiki moja baada ya kufanya tendo la ndoa, majibu yakitoka negative wakati kuna dalili za ujauzito na hakuna hedhi kuna haja ya kurudia tena kipimo baada ya siku saba. Kipimo cha kupima mimba kwa kutumia mkojo kinapatikana kwenye maduka ya dawa muhimu na hujulikana kwa jina la UPT, nhutumika mara moja tu.

WASILIANA NASI KWA UFAHAMU ZAIDI +255757599024-what's app.


No comments

Theme images by compassandcamera. Powered by Blogger.