JINSI YA KUMLAZA MTOTO MCHANGA
- Staili na milalo ya kumlaza mtoto mchanga anapopatwa na usingizi ni kumlaza chali(kwa kulalia mgongo) na kwa ubavu tu mala baada ya kumcheulisha, mtoto mchanga hatakiwi kulala kwa kutumia tumbo anatakiwa alale pekee ake katika sehemu ambayo haina vitu vingi ambavyo vinaweza vikamueka katika hatari ya kupata ajali yoyote.
- Si vizuri kulala kitanda kimoja na mtoto kwani katika usingizi yaweza tokea ukamlalia mtoto au ukamfunika na shuka mtoto kiasi cha kukosa hewa, ni vizuri mtoto akalala pekee ake kwenye kitanda chake lakini ukawa makini kwa kumuangalia hususani usiku, kitanda cha mtoto kinatakiwa kiwe karibu na kitanda cha wazazi kwa ajili ya uangalizi.
- Usimlaze mtoto kifudifudi (kwa kulalia tumbo) kwani huu mlalo waweza sababisha mtoto akakandamiza njia ya hewa hivyo kukosa hewa.
WASILIANA NASI KWA UFAHAMU ZAIDI +255757599024-what's app.
Mungu anatulindia, hivi maisha yetu waafrika tutaweza kumudu kitanda cha mtoto? Asante kwa somo la namna ya kumlaza mtoto.
ReplyDeleteAhsante kwa kutuelimusha
ReplyDeleteMke wangu anapenda sana kumlaza mtoto kifudi fudi nimekuwa nikimkataza sana, ila kwa somo hili imebidi nimuonyeshe na amesoma na kuelewa vzr. Ahsante
ReplyDeleteKaka hata wangu..ila nlichogundua mtoto mchanga hupata usingizi mzuri kwa kulala vile.Japo tu ni hatar endapo kaziuia mfumo wa upumuaj
DeleteThanx
ReplyDeleteAsante kwa somo zuri
ReplyDeleteAhsante kwa somo zuri sana daktari
ReplyDelete