VITU VYA KUFANYA NA KUZINGATIA WAKATI WA UCHUNGU
- Uchungu ni kipindi kigumu kwa mama-mjamzito na ni kipindi ambacho mwanamke yeyote aliyekwisha jifungua hawezi kukisahau katika maisha yake, katika kipindi hiki cha uchungu ni kipindi kinachohitaji, mahusiano mazuri kati ya mamamjamzito na mtoa huduma wa afya, mawasiliano mazuri na ushirikiano wa kutosha kati ya hawa watu ni vitu muhimu katika kipindi hiki cha uchungu, mama mjamzito anatakiwa awe mwerevu, msikivu na anaetoa ushirikiano wa kutosha kwa mtoa huduma ya afya anayemsaidia katika kipindi cha uchungu.
- Hivyo basi ili kipindi hiki kigumu kiweze kuwa chepesi na cha kusaidika mamamjamzito hana budi kufanya au kuzingatia vitu vifuatavyo katika kipindi cha uchungu ili mambo yaweze kuwa mepesi
- Kufanya mazoezi kama vile kutembea, kwenda na uchungu chini ( uchungu ukija chuchumaa chini)

- Kula chakula kipindi cha uchungu, kama vile chai ya moto yenye sukari nyingi, uji, mtoli, vitafunwa, tende, cake, nk.kwa ajili ya nguvu.
- Kuhema(kutoa hewa nje) kila uchungu unapokuja
- Kusikiliza unachoambiwa na kuelekezwa na mkunga/daktari
- Kutokusukuma kabla ya amri; si kila mama mjamzito anapopata uchungu unatakiwa asukume, anatakiwa asubiri mpaka pale atakapopewa amri ya kusukuma
- Kutokubana miguu wakati wa kusukuma
- Kutokusukuma kabla hajapewa amri ya kusukuma, mama mjamzito anatakiwa asukume pale tu anapoambiwa asukume
- Wakati wa kusukuma, mama mjamzito hatakiwi kuachia pumzi katikati ya msukumo.
- Kusukuma kwa nguvu zote; na anapoambiwa kusukuma anatakiwa kusukuma kwa nguvu zote.
- Mama mjamzito anatakiwa Kuwa msikivu na mwerevu wakati wa uchungu pia toa ushirikiano kwa mkunga.
- Hivi vitu vikifanyika na kuzingatiwa wakati wa uchungu basi kipindi hiki cha uchungu kinaweza kutuletea matokeo mazuri ya ujauzito na matokeo mazuri ya ujauzito ni yale yanayo ambatana na kujifungua salama kwa afya ya mama na mtoto pia bila kuwa na matatizo yoyote.
WASILIANA NASI KWA UFAHAMU ZAIDI +255757599024-what's app.
Asante kwa elimu nzuri
ReplyDeleteKaribu
Delete