KIPIMO CHA UJAUZITO (UPT)


Kipimo cha ujauzito hutumika kuthibitisha kama mwanamke ana

 ujauzito baada ya kuwa na dalili ambazo zinaashiria kuwepo kwa

 ujauzito, hiki kipimo hupima uwepo wa hormone ya HCG katika 

aidha mkojo au damu ya mama mjamzito, ambapo hii  hormone 

hutolewa mwilini pale tu mwanamke akiwa mjamzito takribani siku 

6-10 baada ya mimba kutungwa.

                                               
Kama mwanamke hana ujauzito basi hormone ya HCG huwa 

haipatikani kwenye damu na mkojo wa mwanamke, lakini akiwa 

mjamzito hormone ya HCG hupatikana aidha kwenye mkojo au 

damu ya mama mjamzito.
                                               

Ukitaka kupima ujauzito mkojo au damu huchukuliwa, kwa njia ya 

mkojo, mkojo huchukuliwa na kuwekwa kwenye chombo safi 

baadae kipimo huwekwa kwenye chombo chenye mkojo kwa muda 

wa sekunde 10-15 baadae hutolewa kwa kusoma majibu. Kupima 

ujauzito kwa njia ya damu, hii njia hufanyika maaabara tu.

Kipimo huwa na mistari miwili ambapo kikichora mstari mmoja 

huashiria hakuna ujauzito na kikichora mistari miwili huashiria 

uwepo wa ujauzito.


                                   
Muda muafaka wa kutumia hiki kipimo ni pale tu mwanamke 

anapogundua kuwa amekosa damu zake za mwezi na ni vizuri 

kupima mapema au wiki moja baada ya kufanya tendo la ndoa, 

majibu yakitoka negative wakati kuna dalili za ujauzito na hakuna 

hedhi kuna haja ya kurudia tena kipimo baada ya siku saba.
                                               

Kipimo cha kupima mimba kwa kutumia mkojo kinapatikana 

kwenye maduka ya dawa muhimu na hujulikana kwa jina la UPT. 

Na hutumika mara moja tu.


IMEANDALIWA NA BARAKA EDGAR MLALO
REFERENCES
D.C.DUTTA,(2011) Text book of obstetrics, seventh edition, New central book agency(P) ltd, LONDON

GORDON W.GARLAND and ROSEMARY C. PERKES,(1959) A text book for pupil midwives, The english  universities press ltd, LONDON.

LINDA K. BROWN and V.RUTH BENNETH,(1999) Myles textbook for midwives, thirteenth edition, churchill livingstone, EDINBURGH LONDON

No comments

Theme images by compassandcamera. Powered by Blogger.