DALILI ZA YAI KUTOKA KWENYE OVARY NA KUWA TAYARI KWA UCHAVUSHWAJI
- Si kila mwanamke hupata dalili au viashiria vya yai kutoka kwenye ovary, kuna baadhi hupata na wengine hawapati kabisa, na dalili hizi na viashiria haviwapati wanawake kwa muda unaofanana kila mtu hupata kwa wakati wake na kila mtu ana siku yake peke ake ya yai kutoka.
- Ni vizuri kuzijua na kuzitambua dalili hizi kwa ajili ya kujua haswa lini yai linakuwa linatoka au limetoka na tayari kwa uchavushwaji, hii husaidia katika kupanga kwa hiari siku ya kupata ujauzito au kupanga kutopata ujauzito, hivyo ni muhimu kufahamu dalili hizi.
- Ufahamu wa dalili hizi, ufahamu wa mzunguko wa hedhi husaidia kupanga ni wakati gani mwanamke anahitaji kupata ujauzito au ni wakati gani hahitaji kupata ujauzito.
Picha ikionyesha mzunguko wa hedhi na matukio yake
- Baadhi ya dalili za yai kutoka ni;
- Kupatwa na maumivu kama vichomi sehemu za nyonga katikati ya siku za mzunguko wa hedhi
- Matone ya damu kutoka kwenye uke katikati ya mzunguko wa hedhi
- Matiti kujaa katikati ya mzunguko wa hedhi
- Kupata mvurungiko wa tumbo katikati ya mzunguko wa hedhi
- Kupatwa na ongezeko la hamu ya kufanya tendo la ndoa katikati ya mzunguko wa hedhi.
- Kuongezeka kwa ute wa ukeni
- Kutokwa na ute wa ukeni muda wote na ute kubadilika kuwa kama tui jeupe la yai.
- Joto la mwili kuongezeka.
WASILIANA NASI KWA UFAHAMU ZAIDI +255757599024-what's app.




No comments