MUDA MUAFAKA WA KUANZA KUFANYA MAPENZI BAADA YA KUJIFUNGUA

  • Mwanamke anapokuwa mjamzito hupata mabadiliko mbalimbali  ambayo baadhi hutoweka mara baada tu ya kujifungua, mama mjamzito baada ya kujifungua humchukua takriban wiki sita baadhi ya viungo vyake hususani vya uzazi kurudi kawaida kama kabla hajapata ujauzito, hivyo basi mama mjamzito baada ya kujifungua anatakiwa akae takribani wiki sita sawa na mwezi mmoja na nusu ndiyo anaruhusiwa kuanza kufanya mapenzi, huo ndo ushauri wa kitabibu kwa suala la muda upi sahihi wa kuanza kufanya mapenzi baada ya kujifungua. 
  • lakini si lazima kuanza kufanya mapenzi baada ya huo muda kama familia mnaweza kukubaliana muda wenu rasmi wa kuanza kufanya mapenzi lakini usiwe mapema kabla ya wiki sita toka mamamjamzito amejifungua.

  • Kabla ya wiki sita kupita mama aliyetoka kujifungua huwa yuko katika kipindi cha mpito ambapo hupata baadhi ya mabadiliko katika mwili wake ili aweze kurejea kama alivyokuwa kabla ya kupata ujauzito, katika kipindi hiki mama aliyetoka kujifungua hutokwa na uchafu ukeni ulio katika hali ya damu hivyo kuwa katika mazingira magumu ya kufanya mapenzi.
                 
  • Pia katika kipindi hiki viungo vya uzazi hujaribu kurudi katika hali yake ya kawaida, pia ni kipindi ambacho kwa wale walioongezewa njia au waliochanika kwenye uke,  ndo huanza kupona na kurudi kawaida, hivyo ni wakati mgumu sana kwa mama alietoka kujifungua kuanza kufanya mapenzi katika hiki kipindi.
                       
  • Halikadhalika, katika hiki kipindi ni vyepesi sana kwa mama aliyetoka kujifungua kupata maambukizi kama hatazingatia usafi na kuanza kufanya mapenzi kwa kipindi alichopo.Pia mama aliyetoka kujifungua viungo vyake vya uzazi kama vile uke kabla ya muda wa wiki sita huwa havijapona ipasavyo kiasi cha kumfanya apate maumivu kama atafanya mapenzi mapema kabla ya muda wa wiki sita, pia kwa mama anayenyonyesha sehemu zake za siri huwa kavu kiasi cha kumfanya kupata maumivu endapo ataamua kufanya mapenzi mapema.
                         
  • Hata baada ya wiki sita kuisha mama aliyetoka kujifungua anaruhusiwa kuanza kufanya mapenzi hivyo basi anatakiwa pia kuwa ameshachagua njia ya uzazi wa mpango kwani anaweza pata ujauzito kwa muda wowote atakapoanza kufanya mapenzi, kama familia ni vizuri kutambua, kuamua na kupanga njia sahihi ya uzazi wa mpango watakayo tumia baada ya mamamjamzito kujifungua. Onana na watoa huduma wa afya kwa ushauri mzuri juu ya njia sahihi ya uzazi wa mpango.

WASILIANA NASI KWA UFAHAMU ZAIDI +255757599024-what's app.

No comments

Theme images by compassandcamera. Powered by Blogger.