JINSI YA KULALA MAMA-MJAMZITO.

  • Mwanamke anapokuwa mjamzito ni tofauti sana na kipindi hana ujauzito, mambo mengi hutokea kipindi cha ujauzito ambayo hubadilisha maisha ya kawaida ya mwanamke na kumfanya kubadili baadhi ya tabia au mwenendo wa maisha yake. Baadhi ya mambo ambayo mama-mjamzito hutakiwa kubadilika ni pamoja na aina ya kulala kipindi cha ujauzito.

  • Mwanamke anapokuwa mjamzito na kadri mimba inavyokuwa tumbo lake huongezeka ukubwa, ukuaji wa mimba hutofautiana katika vipindi vitatu vya ujauzito; miezi mitatu ya kwanza mimba inakuwa badoo iko kwenye nyonga haijafika kwenye tumbo, miezi mitatu ya katikati na ya mwisho, mimba inakuwa kwenye tumbo na kufika kwenye kifua hali hii humpelekea mama-mjamzito apate shida ya kulala, kupumua, kutembea hata kupata maumivu ya mgongo na nyonga. 
  • Ukubwa wa tumbo unaosababishwa na uwepo wa mtoto/watoto tumboni mwa mama, husababisha mama-mjamzito akatazwe kulala baadhi ya milalo kama vile; chali (kulalia mgongo), na kifudifudi (kulalia tumbo). Hii milalo imekatazwa kwasababu, mama akilala chali mtoto hukandamiza mshipa wa damu hivyo kusababisha msukumo wa damu wa chini (hypotension), akilala kifudifudi husababisha mama kutojisikia vizuri.

  • Hivyo basi kutokana na hayo madhara, mama-mjamzito anashauliwa kulala mlalo wa ubavu tu katika kipindi kizima cha ujauzito, anashauliwa alale zaidi ubavu wa kushoto kuliko ubavu wa kulia. Pia wakati amelala kwa ubavu anashauliwa kutumia mito, mito hii anashauliwa kuiweka katikati ya miguu, chini ya tumbo na kichwa chake, hii humsaidia mama-mjamzito asipatwe na kiungulia, maumivu ya nyonga, mgongo, miguu na asichoke sana.

WASILIANA NASI KWA UFAHAMU ZAIDI +255757599024-what's app.

No comments

Theme images by compassandcamera. Powered by Blogger.