DALILI HATARISHI KWA AFYA YA MTOTO MCHANGA.

Mtoto mchanga ni nani?

  • Mtoto mchanga ni mtoto mwenye umri wa siku 28 baada ya kuzaliwa, afya ya mtoto mchanga huzidi kuimalika kadri anavyozidi kukuwa. Mtoto mchanga anapokuwa na tatizo lolote la ki-afya au anapokuwa anaumwa, ni vigumu kwa mzazi au mlezi kufahamu kwasababu mtoto hawezi ongea anachohisi mwilini mbali huyu mtoto ataonyesha ishara au dalili zinazoashilia kuwa kuna kitu mwilini kinamsumbua na angependa kupatiwa msaada.

  • Hivyo basi ni jukumu la mzazi au mlezi kuweza kuzifahamu hizo dalili ili aweze kuzitambua kipindi pale mtoto atakapozionyesha, hizi ni baadhi ya hatarishi ambazo zikionekana kwa mtoto basi huashiria kuwa mtoto anaumwa au anashida na angependa kupewa huduma ya afya.
      • Kutokuwa na hamu ya chakula au kukataa kula chakula
      • Mwili wake kupata joto kali
      • Kupata dege dege
      • Kupoteza fahamu
      • Kupumua kwa haraka/kupumua kwa shida
      • Kutohisi kitu chochote, mfano akishituliwa
      • Kutoa sauti akiwa ana pumua
      • Kuwa wa baridi sana
      • Mwili wake kuwa wa njano
      • Kutopata choo ndani ya masaa 24
      • Kulia bila sababu inayoweza kujulikana
      • Uso wake kuwa wa bluu

WASILIANA NASI KWA UFAHAMU ZAIDI +255757599024-what's app.

No comments

Theme images by compassandcamera. Powered by Blogger.