JINSI YA KUMUAMSHA MTOTO MCHANGA USINGIZINI.

  • Mtoto mchanga anapotoka kuzaliwa anakuwa amechoka na huhitaji kupumzika, huhitaji masaa 14-17 ya kulala ndani ya siku moja, japokuwa wengine hulala mpaka masaa 18-19, na usingizi wao huwa wa muda mfupi masaa 2-3 ambao hauna wakati maalum, inaweza kuwa mchana au usiku. 

  • Japokuwa muda wake mwingi hutumia kulala, hii hali inaweza kuingiliana na muda wa kunyonya maziwa, pia kuanzisha mahusiano baina yake na wazazi wake. Hivyo basi kwa mtoto anaekuwepo amelala lakini akawa anahitajika kunyonya kwa wakati huo, mzazi hana budi kumuamsha toka usingizini na kumlisha.
  • Kwasababu mtoto anakuwa amelala, hairuhusiwi kumuamsha kwa kupiga kelele, kumpiga au kumfinya, kwani kufanya hivyo humuogopesha mtoto na kumuondolea utulivu na amani. Hizi ni baadhi ya njia ambazo hutumika kumuamsha mtoto aliye lala usingizini.

    • Kumsungua polepole kwenye paji la uso
    • Kumtekenya kwenye viganja vya mikono na miguu
    • Kumsungua kwenye viganja vya miguu
    • Kumpiga taratibu kwenye kwa kutumia kidole kwenye viganya vya miguu.
WASILIANA NASI KWA UFAHAMU ZAIDI +255757599024-what's app.

No comments

Theme images by compassandcamera. Powered by Blogger.