UZAZI WA MPANGO (FAMILY PLANNING).
- Uzazi wa mpango ni kutambua, kuamua, na kupanga idadi ya watoto ambao, wanandoa au mtu atakao weza kuwalea katika mpangilio ulio bora kwa ajiri ya afya zao na wazazi pia. Uzazi wa mpango hujumuisha kutoa ushauri nasaha kuhusu mpangilio wa watoto na umuhimu wake, pia matumizi, faida, ufanisi na maudhi ya njia za uzazi wa mpango.
- Uzazi wa mpango unawapa uhuru wanandoa au mtu kuamua na kuchagua idadi ya watoto wanaowahitaji na kupanga kuwapata katika muda walioamua kuwapata. Kuamua na kupanga idadi ya watoto katika muda muafaka hutimia kwa kutumia njia mbalimbali za uzazi wa mpango zilizohidhinishwa kwa lengo la kusaidia watu wanaotumia uzazi wa mpango. Njia hizi ni kama vile; sindano, vidonge, kitanzi, kipandikizi na kondom, pia kukatwa au kuzibwa mirija ya uzazi.
- Huduma ya uzazi wa mpango ni huduma ya kila mtu aliyeko kwenye umri wa uzazi (15-49) anayehitaji kupanga uzazi, si huduma ya wanandoa tu au watu wazima tu, ni huduma inayohusisha hata vijana.
FAIDA ZA UZAZI WA MPANGO.
- Husaidia kuzuia mimba za utotoni kwa vijana wanaotumia njia za uzazi wa mpango.
- Husaidia kupunguza uhitaji wa utoaji wa mimba.
- Husaidia kupunguza idadi ya mimba zisizohitajika na kutarajiwa.
- Baadhi ya njia za uzazi wa mpango hutoa kinga dhidi ya magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiana (ngono).
- Hoboresha afya ya familia.
WASILIANA NASI KWA UFAHAMU ZAIDI +255757599024-what's app.
No comments