DALILI ZA UCHUNGU/KUTAKA KUJIFUNGUA.
- Uchungu ni hali ya mama mjamzito kujihisi anataka kujifungua ambayo huambatana na maumivu makali ya tumbo, hali hii inapoanza hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke. Uchungu unaweza kuanza muda wowote sehemu yoyote, pia unaweza kuanza kabla, wakati au baada ya tarehe ya makadilio.
- Uchungu huanza wenyewe au kama haujaanza basi huanzishwa, na mimba ikitaka kutoka au mama-mjamzito akitaka kujifungua lazima apate uchungu. Uchungu lazima uwepo ili mama mjamzito aweze kujifungua au mimba iweze kutoka. Ili uchungu uitwe uchungu, mama-mjamzito huonyesha dalili kuashilia kuanza kwa hatua ya kujifungua, hizi dalili huwasaidia watoa huduma za afya katika utoaji wa huduma sitahiki.
- Hizi ni baadhi ya dalili za uchungu ambazo mama-mjamzito akizipata basi hanabudi kuonana na watoa huduma za afya;
- Ongezeko la majimaji ukeni; mwanamke anapokuwa mjamzito majimaji ya ukeni huongezeka, na uchungu unapoanza haya majimaji ya ukeni huongezeka zaidi na wakati mwingine huweza kulowanisha nguo za ndani.
- Show; huu ni ute mzito uliochanganyikana na damu na kuupa rangi ya brown (ugoro), huu ute hukaa kwenye shingo ya uzazi kipindi cha ujauzito kwa kuzuia maambukizi yasiingie kwa mtoto, uchungu unapoanza huu ute hutoka nje na kuonekana kwenye uke, hivyo kuashilia kwamba uchungu umeshaanza.
- Maumivu ya tumbo yasiyoeleweka; katika kipindi cha mwisho cha ujauzito, mama-mjamzito hupatwa na maumivu ya tumbo yasiyo makali na yasiyoeleweka, haya maumivu ya tumbo hutokea kwa wingi kwenye kipindi cha mwisho cha ujauzito (miezi mitatu ya mwisho) na huashilia kuanza kwa hatua za uchungu.
- Maumivu makali ya tumbo; mama-mjamzito akipatwa na maumivu makali ya tumbo yanayokuja na kuondoka na kudumu kwa muda wa sekunde 30 au zaidi, na kupishana kwa kila dakika 5 au 10, haya maumivu ya tumbo huashilia maumivu ya uchungu na ni dalili mojawapo za kuanza kwa uchungu.
- Maumivu ya mgongo; maumivu ya uchungu wa kweli huambatana na maumivu ya mgongo sana sana sehemu ya kiunoni.
- Chupa ya uzazi kupasuka; katika kipindi cha ujauzito, mtoto kwenye tumbo la uzazi huwa amezungukwa na maji yanayomlinda na hatari mbalimbali, maji hayo yanakuwa ndani ya chupa au mpira, hii chupa hupasuka ili mtoto azaliwe, upasukaji wa hii chupa unaweza kutokea kabla ya uchungu, wakati wa uchungu au kuwakati wa kuzaa, hivyo basi upasukaji wa hiyo chupa huashilia kuwa uchungu umeshaanza. Japokuwa muda mwingine uchungu unaweza kuanza wakati chupa bado haijapasuka.
- Kujihisi/kupata unafuu kwenye kifua na maumivu ya mgongo; mtoto anapokuwa tumboni kwa mama-mjamzito na kabla hajaanza kushuka chini kwenye nyonga huwa anakandamiza msuli wa upumuaji unaoitwa diaphragm hivyo kumfanya mama-mjamzito kupatwa na shida ya upumuaji. Lakini uchungu unavyoanza na mtoto kushuka chini ya nyonga, uzito uliokuwepo kwenye msuli wa upumuaji hupungua hivyo kumfanya mama kuhisi wepesi kifuani na maumivu ya mgongo kupungua, hii huanshilia kuanza kwa hatua za uchungu.
- Kuharisha; uchungu huambatana na mama-mjamzito kuharisha
- Ongezeko la haja ndogo; uchungu unapoanza humpelekea mama-mjamzito kuwa anapata hali ya haja ndogo mara kwa mara.
- Mama-mjamzito afike kituo cha afya kilichopo karibu akiona baadhi ya dalili hizo hapo juu.
WASILIANA NASI KWA UFAHAMU ZAIDI +255757599024-what's app.
No comments