UTOAJI MIMBA NA NJIA ZAKE (ABORTION).
- Kwa sheria ya Tanzania utoaji mimba ni kosa la jinai na hairuhusiwi kwa mwanamke kutoa mimba, mtoaji na mtu aliyeshiriki katika kusaidia kwa njia yeyote ile zoezi zima la utoaji mimba hushitakiwa kwa kosa la jinai. Lakini sheria hii inaruhusu utoaji mimba katika hali ambayo mimba inahatarisha uhai wa mama-mjamzito, katika hali hii daktari hupewa kibali cha kutoa huo ujauzito lakini mpaka ithibitishwe na jopo la madaktari bingwa.
- Ukiachana mbali na sheria, utoaji mimba ni hali ya kuamua kukatisha maendeleo ya ujauzito yasifikie katika hatua ya kupata mtoto. Japokuwa nchini tanzania sheria inakataza suala zima la utoaji mimba, lakini kwa nchi za nje zinaruhusu utoaji mimba kwa ujauzito ambao upo chini ya wiki 28. Utoaji wa mimba katika nchi hizo unaruhusiwa katika hali ambayo ujauzito umepatikana bila kupangwa au mwenye ujauzito hautaki tena.
- Kutengemea na umri wa ujauzito njia mbili hutumika kataika utoaji mimba;
- Utoaji mimba kwa vidonge.
- Utoaji mimba kwa vifaa.
UTOAJI MIMBA KWA VIDONGE.
- Katika hii njia mimba hutolewa au hukatishwa maendeleo yake kwa kutumia vidonge. Na hii njia huwa na matokeo mazuri kwa ujauzito ulio chini ya wiki 12. Ambapo katika hii njia muhusika hutumia vidonge mahususi kwa ajiri ya kutoa mimba, si kila vidonge huweza kutoa mimba. Kabla ya utumiaji wa hivyo vidonge, mtoaji anatakiwa kufanya kipimo cha ultrasound kuhakikisha kama ujauzito upo ndani ya kizazi, na wingi wa damu yake.
- Mtoaji anatakiwa kupima kipimo cha ujauzito mara baada ya siku 14 ili kudhibitisha kama mimba imetoka kweli, kama itakuwa haijatoka mtoaji anaruhusiwa kutumia vidonge vingine, utumiaji wa vidonge hivyo huambatana na maumivu makali ya tumbo, kuharisha, kichefuchefu, kutapika, damu kutoka nyingi, kizunguzungu na homa. Wanawake wenye upungufu wa damu, mimba nje ya kizazi, mimba ya mapacha, ugonjwa wa kutokwa na damu nyingi, na waliopo kwenye matumizi ya dawa za kuyeyusha damu hawaruhusiwi kutumia hivyo vidonge.
UTOAJI MIMBA KWA VIFAA.
No comments