SARATANI YA MATITI (BREAST CANCER).
- Saratani ya titi (matiti) hutokana na ukuaji wa seli uliopitiliza kipimo kulingana na inavyotakiwa hivyo kupelekea kutokea kwa uvimbe ndani ya titi au matiti ya mwanamke au mwanaume. Uvimbe unaosababisha saratani ya titi huanza katika sehemu mbalimbali za titi, lakini mara nyingi huanzia kwenye mirija inayosafirisha maziwa kutoka kwenye tezi kwenda kwenye chuchu. Sio uvimbe wote kwenye titi unasababisha au kumaanisha saratani, baadhi ya uvimbe ndani ya titi hauhusiani na saratani.
SABABU HATARISHI ZA SARATANI YA TITI.
- Kuwa na jinsia ya kike.
- Mwanamke mwenye umri mkubwa.
- Mwanamke mwenye historia ya kupata saratani ya titi.
- Mwanafamilia mmoja kuwahi kupata saratani ya titi.
- Mwanamke mwenye vinasaba vya kurithi vya saratani ya titi.
- Mwanamke anayefanya kazi kwenye mionzi.
- Mwanamke mwenye unene uliopitiliza.
- Mwanamke aliyevunja ungo mapema chini ya miaka 12.
- Mwanamke aliyechelewa kukoma hedhi baada ya miaka 55.
- Mwanamke aliyechelewa kuzaa mtoto wa kwanza baada ya miaka 35.
- Mwanamke ambaye hajawahi kushika ujauzito.
- Mwanamke anayetumia matibabu ya vichocheo (hormones) baada ya kukoma hedhi.
- Mwanamke anayetumia pombe na sigara.
- Mwanamke akiwa na hizo sababu zilizotajwa hapo juu haimanishi ndo ameshapata saratani ya titi lahasha, bali humuweka mwanamke katika hatari ya kupata saratani ya titi ukilinganisha na mwanamke ambaye hana hizo sababu.
DALILI ZA SARATANI YA TITI/MATITI.
- Uvimbe au kitu kingumu kisichofanana na kitu kingine ndani ya titi au kwenye kwapa
- Titi kujaa au kuwa kubwa, la moto, jekundu au jeusi
- Kubadilika muonekano na ukubwa wa titi.
- Ngozi ya titi kuwa na dimpozi au kama ganda la chungwa
- Titi kuwasha au kuwa na viupele na kutokwa na vidonda
- Chuchu au sehemu nyingine ya titi kuingia ndani
- Chuchu ya titi kutoa majimaji
- Maumivu makali katika sehemu moja ya titi, ambayo hayaishi na hayasikii dawa.
- Kujizuia unywaji pombe
- Kutovuta sigara
- Kujizuia kuongezeka uzito
- Kufanya mazoezi ya mwili
- Unyonyeshaji maziwa ya mama kwa kutumia matiti
- Kupunguza dozi/matumizi ya vochocheo (hormones) mbadala baada ya kukoma hedhi.
- Kujizuia na mionzi hatarishi
- Kufanya ukaguzi wa matiti kila baada ya hedhi.
UKAGUZI WA MATITI MWENYEWE.
- Saratani ya titi/matiti inaweza kuzuirika kama itagundulika mapema, mwanamke anajukumu la kujikagua viashiria vya uvimbe kwenye matiti yake kila amalizapo hedhi, wakati wa ukaguzi hivi ni vitu ambavyo mwanamke anatakiwa kuvizingatia.
- Muonekano, ukubwa na rangi ya matiti.
- Ngozi ya titi isiyokuwa na dimpozi au kufanana na ganda la chungwa.
- Chuchu iliyoingia ndani na inayotoa majimaji.
HATUA ZA KUFATA WAKATI WA UKAGUZI.
- Mwanamke anatakiwa aanze kujiangalia kwenye kioo akiwa hana nguo huku mabega yake yakiwa yamenyoka na mikono imeshika kiuno.
- Taratibu anyoshe mikono yake juu huku akiangalia kwenye kioo kama matiti yake yote yanapanda juu kwa pamoja.
- Wakati akiwa anajiangalia, pia aangalie chuchu zake kama zinatoa; majimaji, maziwa au damu.
- Akimaliza hizo hatua za kujiangalia, anatakiwa alale chini kwa kutumia mgongo (chali), aweke mkono wa kushoto chini ya kichwa na atumie mkono wa kulia kukagua uvimbe kwenye titi la kushoto, hivyo hivyo pia kwenye mkono wa kulia. wakati wa ukaguzi anatakiwa atumie vidole vyake vinne kushika titi taratibu kuanzia kwenye chuchu kuelekea pembeni mwa titi kwa mzunguko.
- Mwisho mwanamke asimame na kunyosha mkono wake wa kulia na kutumia mkono wa kushoto kukagua titi la upande wa kulia, hivyo hivyo kwa mkono wa kushoto pia. Akiwa anafanya ukaguzi ajitahidi kuangalia uvimbe kwenye titi husika, na atumie vidole vyake vinne kushika titi kuanzia kwenye chuchu kuelekea pembeni mpaka kwenye kwapa kwa mzunguko.
WASILIANA NASI KWA UFAHAMU ZAIDI +255757599024-what's app.
No comments