DALILI HATARISHI KIPINDI CHA UJAUZITO

  • Ujauzito ni kitu kizuri kuwahi tokea katika maisha ya mwanamke pia ni baraka za mwenyezi mungu lakini uwepo wa ujauzito kwa kipindi chote cha ujauzito hutegemea pia kudura za mwenyezi mungu. Ujauzito huambatana na mambo mbalimbali yanayoathiri afya ya mama katika kipindi cha ujauzito, maendeleo mazuri ya ujauzito hutegemea na afya ya mama-mjamzito, ndo maana mwanamke anatakiwa aijue vizuri afya yake kabla na baada ya kupata ujauzito. 
  • Ujauzito ukitaka kutoka au kuharibika mwili hutoa baadhi ya viashiria ambavyo huitwa dalili hatarishi kipindi cha ujauzito, mama mjamzito akipatwa na miongoni mwa hizo dalili katika kipindi chochote cha ujauzito, ni vizuri akaonana na watoa huduma za afya ili kuweza kupata huduma husika kutokana na tatizo husika. Baadhi ya hizo dalili ni; 

    • Kutokwa na damu ukeni.
    • Maumivu tumbo la chini yakiambatana na kutokwa na damu ukeni.
    • Maumivu makali ya tumbo pembeni ya nyonga yanayoenda mpaka mgogoni au kwenye bega.
    • Kichefu chefu na kutapika kuliko pita kiasi.
    • Mtoto kupunguza kucheza au kutokucheza kwa muda wa siku 1 baada ya mimba kufikisha wiki 20..
    • Chupa ya uzazi kupasuka pasipo na uchungu au kabla tarehe ya makadilio.
    • Uchungu kuanza kabla ya tarehe ya makadilio.
    • Kuugua kipanda uso.
    • Kupata maluelue.
    • Kuanguka kifafa.
    • Kuvimba mwili na miguu.
    • Kupata msukumo wa damu zaidi ya 140/90.
    • Maumivu sehemu ya juu ya tumbo.
    • Kupata aina yoyote ya ajari.
    • Kupata maambukizi ya ukeni au magonjwa ya zinaa.
      WASILIANA NASI KWA UFAHAMU ZAIDI +255757599024-what's app.

No comments

Theme images by compassandcamera. Powered by Blogger.