UNYONYESHAJI WA MTOTO.
- Mtoto anapokuwa tumboni hutegemea kila kitu kutoka kwa mama yake, chakula ni moja ya vitu ambavyo mtoto hutegemea, katika kipindi cha ujauzito kila kitu mama-mjamzito akilacho humfikia mtoto kwa njia ya damu na husaidia katika maendeleo na ukuaji. Hivyo basi kwa kipindi chote cha ujauzito takribani miezi 9, mtoto hutegemea lishe ya mama yake ili kupata virutubisho muhimu. Baada tu yakujifungua na kitovu cha mtoto kukatwa, mtoto huanza maisha yake na kuacha kutegemea kwa mama, katika hiki kipindi mtoto hupata virutubisho kwa kunyonya maziwa ya mama, hivyo huhitaji kunyonyeshwa ili aweze kupata virutubisho muhimu vya kumsaidia kwenye ukuaji na maendeleo yake.
- Mara baada ya kujifungua, mama anatakiwa aanze kumnyonyesha mtoto wake ndani ya saa moja, na kwa kipindi cha miezi 6 toka amejifungua mtoto hatakiwi kula au kunywa kitu chochote kile zaidi ya maziwa ya mama. Baada ya miezi sita mama anaruhusiwa taratibu kuanza kumpa maziwa na baadhi ya vyakula lakini visivyo vigumu; vilivyo kwenye hali ya kimiminika kama vile maji, supu, mtori, uji, minofu ya samaki nk. katika kipindi cha unyonyeshaji, maziwa ya mama ndo chakula pekee cha mtoto, na anatakiwa akipate hiki chakula si chini ya miaka 2, japokuwa maziwa ya kopo hutumika kama mbadala katika hali ambazo mama inambidi; mara baada ya kujifungua akina mama hukaa baadhi ya siku chache matiti hayatoi maziwa katika hiki kipindi mama anaruhusiwa kumnyonyesha mtoto maziwa ya kopo.
- Mama anatakiwa amunyonyeshe mtoto pale anapohitaji au kila baada ya masaa 3 au 2 na kwa kila mnyonyo mtoto anatakiwa anyonye ziwa mapaka pale atakapoacha mwenyewe au dakika 10-40. Unyonyeshaji unaweza kuwa kwenye titi, kikombe au chupa kwa wale wanaokamua maziwa.
VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA UNYONYESHAJI.
- Mtoto anatakiwa aanze kunyonyeshwa ndani ya dakika 30 mara baada tu ya kujifungua.
- Mtoto anatakiwa anyonye kila baada ya masaa 3 au 2 sawa na mara 8 au 12 kwa siku.
- Wakati wa kunyonyesha mtoto, mama anatakiwa kuonyesha upendo kwa mtoto; ongea uso kwa uso na mtoto, tabasamu, nk.
- Usitumie chupa, au kijiko kumlisha mtoto maziwa, tumia kikombe kisafi kwa wale wanaomlisha mtoto maziwa ya kopo au wanaokamua maziwa.
- Hakikisha mtoto ananyonya sehemu nyeusi ya titi na sio chuchu ya ziwa.
- Wakati wa unyonyeshaji mama anatakiwa ahakikishe mtoto hatoi sauti akiwa ananyonya, hii huashilia kuwa mdomo wa mtoto na ziwa la mama havijakaa vizuri.
- Mtoto anatakiwa acheulishwe kila baada ya kunyonya.
- Mama anatakiwa kuepuka mawazo katika kipindi cha unyonyeshaji, hali hii hupunguza utokaji wa maziwa.
- Kuumwa, na kutokula chakula cha kutosha na utumiaji wa baadhi ya dawa, husababisha pia upungufu wa maziwa.
FAIDA ANAZOPATA MAMA-MNYONYESHAJI.
- Mama anayenyonyesha hupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa kisukari.
- Mama anayenyonyesha hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya titi na ovary.
- Unyonyeshaji humsaidia mama kurudisha uzito wake kabla ya kubeba ujauzito.
- Unyonyeshaji husaidia mama kuanzisha na kujenga uhusiano mzuri na mtoto.
- Unyonyeshaji humsaidia mama kuchelewa kuanza mzunguko wake wa hedhi mara baada ya kujifungua, lakini hii ni kwa wale wanaonyonyesha mara kwa mara.

No comments