MAZOEZI KIPINDI CHA UJAUZITO.
- Mama mjamzito anatakiwa afanye mazoezi katika kipindi cha ujauzito, ikiwa tu ujauzito wake hauna matatizo, au ukiwa hauambatani na magonjwa yanayo hatarisha maendeleo ya ujauzito wake. Kwa akina mama waliokuwa wanafanya mazoezi kabla ya kupata ujauzito wanashauriwa kuendelea kufanya mazoezi katika kipindi cha ujauzito, lakini wanatakiwa kupunguza kiwango na muda wa kufanya hayo mazoezi.
- Nakala mbalimbali zinashauri mama-mjamzito anatakiwa angalau kwa wiki afanye mazoezi mara 1 au 2 kwa muda wa dakika 30. Pia anashauriwa kabla ya kuamua kufanya mazoezi, ni vizuri akaonana na daktari ili aweze kuangalia kama ujauzito hauna matatizo yoyote na haujaambatana na magonjwa yanayo hatarisha maendeleo ya huo ujauzito.
- Matatizo na magonjwa ambayo mama-mjamzito akiwa nayo hatakiwi kufanya mazoezi au akiyapata wakati akifanya mazoezi anatakiwa kuacha mara moja;
- Historia ya kutoa mimba.
- Historia ya chupa ya uzazi kupasuka kabla ya uchungu.
- Historia ya kupata uchungu kabla ya tarehe ya makadilio.
- Kondoo la nyuma (placenta) kukaa kwenye mlango wa uzazi.
- Historia ya kuzaa mtoto njiti.
- Kutokwa na damu kwenye uke.
- Mama-mjamzito mwenye ugonjwa wa pumu.
- Mama-mjamzito mwenye msukumo wa damu mkubwa.
- Mama-mjamzito mwenye shingo ya uzazi isiyo imara.
MAZOEZI YA KUFANYA KIPINDI CHA UJAUZITO.
- Kuogelea; ni mojawapo wa zoezi ambalo mama-mjamzito anashauriwa kufanya, zoezi hili ni salama kwa mama-mjamzito na mtoto kwasababu halimsababishi mama-mjamzito kuanguka, na humsaidia kujenga pumzi na stamina. Mama-mjamzito afanye hili zoezi kama tu anajua kugelea na kabla ya kushika ujauzito alikuwa anaweza kuogelea.
- Kutembea; ni zoezi linaloshauriwa sana kufanyika katika kipindi cha ujauzito, zoezi hili ni salama na husaidia damu kuzunguka mwili mzima, hivyo kuondoa uchovu na kuongeza hali.
- Yoga; mazoezi ya yoga hufanyika kuleta uimara wa mwili, utulivu wa akili, na upumuaji mzuri, mama-mjamzito anashauriwa pia kufanya haya mazoezi, katika kipindi cha ujauzito haya mazoezi husaidia mama-mjamzito kutengeneza pumzi, huongeza uwezo wa kupumua, huondoa uchovu, wasiwasi na kukaza misuli ya uzazi.
- Kegel; ni mazoezi rahisi kufanyika, hayahitaji nguvu, hayatumii muda mrefu na yanaweza fanyika sehemu yoyote ile kwa wakati wowote ule, haya mazoezi hufanyika kwa lengo la kuimarisha misuli ya uke na uzazi. kabla hayajafanyika hakikisha kibofu hakina mkojo, sehemu ulipo, bana misuli ya uke kwa kufanya kama vile unazuia mkojo usikutoke kwa muda wa sekunde 30 achia na rudia tena, fanya mara nyingi uwezavyo wakati wa ujauzito, endelea hata baada ya kujifungua.
- Kucheza muziki; pia hili ni zoezi linaloshauriwa wakati wa ujauzito, zoezi hili huamsha hisia hivyo kusaidia kuondoa wasiwasi, uchovu na kutuliza akili kipindi cha ujauzito, zoezi hili pia huimarisha uhusiano wa familia pale mke na mme au mwenza wanapoamua kucheza pamoja.
VITU VYA KUZINGATIA WAKATI WA MAZOEZI.
- Mama-mjamzito anatakiwa avae nguo na viatu vya mazoezi.
- Mama-mjamzito hatakiwi kubana pumzi wakati akifanya mazoezi.
- Mama-mjamzito hatakiwi kufanya mazoezi zaidi ya dakika 30.
- Mama-mjamzito hatakiwi kufanya mazoezi ya kulalia tumbo.
- Mama-mjamzito asifanye mazoezi yatakayomfanya alalie mgongo kwa muda mrefu.
- Mama-mjamzito asifanye mazoezi ya kucheza mpira, kuruka kamba, na kukimbia.
UMUHIMU WA MAZOEZI KIPINDI CHA UJAUZITO.
- Mazoezi kipindi cha ujauzito yana umuhimu wake kwa afya ya mama- mjamzito na mtoto pia, mazoezi humsaidia mama-mjamzito;
- Kujenga na kuimarisha afya yake kipindi cha ujauzito.
- Kupunguza uwezekano wa kupata kisukari cha mimba.
- Kupata usingizi mzuri.
- Kutopata maumivu ya mgongo kipindi cha ujauzito.
- Hupunguza uwezekano wa kupata choo kigumu.
- Huupa mwili nguvu na hali nzuri ya mwili.
- Hukomaza na kuipa uimala misuli ya uzazi.
- Husaidia kurudisha umbo na viungo vya uzazi katika hali yake ya kawaida kwa haraka zaidi mara baada ya kujifungua.
No comments