SARATANI YA MLANGO WA UZAZI.


Ni saratani ambayo hutokea na kuanzia kwenye shingo ya uzazi ya 

mwanamke ambayo isipogundulika na kutibiwa mapema husambaa 

katika viungo mbalimbali vya mwili na huweza sababisha kifo kwa 

mama alie na hio saratani.

Saratani hii husababishwa na kirusi aitwaye human papilloma virus 

(HPV) ambaye hupatikana kwenye maumbile ya kiume au viungo 

vya uzazi vya kiume(uume), hiki kirusi huweza kusambazwa kwa 

njia ya kujamiana, sana sana kujamiana bila kutumia kinga yoyote 

ile yaani kushiriki ngono zembe katika umri mdogo.

Hiki kirusi kwa mwanaume hakina madhara na kinaishi kwenye 

viungo vyake vya uzazi, madhara kwa mwanamke hutokea pale tu 

kinapokuwa kwenye maumbile ya uzazi ya kike (mlango wa uzazi) 

ila kwa mwanaume wanaweza kupata madhara yanayosababishwa 

na hiki kirusi kwa wale wanaume waliokwenye mahusiano ya jinsia 

moja na kushiriki ngono kwa njia ya mdomo ambapo wakipata 

maambukizi ya hiki kirusi huweza kupata saratani ya koo la hewa.

Saratani ya mlango wa uzazi inatibiwa pale tu inapogudulika 

mapema  na kabla haijasambaa kwenye viungo mbalimbali vya 

mwili, maambukizi huanza kwenye mlango waa uzazi mengine 

huweza kupotea bila matibabu yoyote yale lakini mengine huweza 

kuendelea na yasipo gundulika mapema na kupatiwa matibabu huwa 

saratani na baadae kusambaa mwilini mwisho husababisha kifo.

Habari nzuri kuhusu saratani ya mlango wa uzazi ni kwamba ina 

chanjo, inatibika na inagundulika mapema kama mtu akifanyiwa 

uchunguzi na huduma ya uchunguzi inapatikana katika hospitali 

kubwa kama vile KCMC, MUHIMBILI NA BUGANDO. Ni vizuri 

kufanya uchunguzi mapema hata kama huna dalili za saratani hii.


IMEANDALIWA NA BARAKA EDGAR MLALO AFISA MKUNGA (BSc MIDWIFERY)

REFERENCES;
Gynecology by ten teacher 18th edition






No comments

Theme images by compassandcamera. Powered by Blogger.