MAZIWA YA MAMA
- Maziwa ya mama ni maziwa yanayotengenezwa na yanayotoka katika matiti ya mwanamke kwa ajili ya kumlisha au kama chakula kwa mtoto aliyezaliwa.
- Maziwa ya mama ni chakula cha mwanzo cha mtoto mchanga kabla hajaweza kula au kutumia aina nyingine za vyakula, haya maziwa ya mama yana kila aina ya virutubisho vinavyomwezesha mtoto mchanga asiweze kula aina ya chakula chochote kile kwa muda wa miezi sita.
- Ukiachana na virutubisho vilivyo kwenye maziwa ya mama, maziwa ya mama
pia yana kinga za mwili ambazo humsaidia mtoto kujikinga na maradhi mbalimbali angali akiwa mtoto.
- Pia maziwa ya mama humuepusha mtoto asipatwe na mzio (allergy) mbalimbali ya vyakula.
- Maziwa ya mama yamegawanyika kutokana na vipindi vya utokaji au unyonyeshaji.
- Colostrum; haya ni maziwa ya mama ambayo huanza kutoka pindi tu pale mwanamke anaposhika ujauzito mpaka siku tatu au nne baada ya kujifungua. haya maziwa huwa mazito na yana rangi ya njano. colostrum au maziwa ya mwanzo, huwa yana wingi wa protein, kinga za mwili, vitamins na madini ya mwili, ambavyo hivi vyote ni muhimu katika ukuaji na maendeleo mazuri ya mtoto.
- Maziwa ya mpito; haya ni maziwa ambayo huanza kutoka baada ya siku nne toka kuzaliwa kwa mtoto, haya maziwa huwa mepesi, mazito na yenye rangi nyeupe. maziwa haya ambayo hutoka baada ya colostrum, huwa yana wingi wa virutubisho vya mafuta, wanga, protein na vitamins. maziwa ya mwanzo (colostrum) na ya mpito ni muhimu sana kwa kichanga na humsaidia mtoto katika ukuaji na humkinga na maradhi mbalimbali.
- Maziwa halisi; haya maziwa huanza kutoka takribani siku ya kumi mpaka kumi na tano (10-15), toka mama ajifungue mtoto, maziwa haya hudumu kwa kipindi chote cha unyonyeshaji. haya maziwa hubadilika kwa wingi wa virutubisho katika kipindi cha unyonyeshaji, mtoto anapokuwa anaanza kuinyonya haya maziwa yanakuwa na wingi wa maji na huwa ya blue kwa rangi, lakini kadri mtoto anavyo endelea kunyonya maziwa huwa yanakuwa na wingi wa mafuta na huwa yanakuwa na rangi nyeupe. ni jukumu la mama kuhakikisha mtoto anapata aina ya maziwa yote katika kila kipindi cha unyonyeshaji kwa kutombadilisha mtoto titi wakati ananyonya.
WASILIANA NASI KWA UFAHAMU ZAIDI +255757599024-what's app.
No comments