VITU VYA KUFANYA NA KUZINGATIA WAKATI WA UCHUNGU


Uchungu ni kipindi kigumu kwa mamamjamzito na ni kipindi 

ambacho mwanamke yeyote aliyekwisha jifungua hawezi kukisahau 

katika maisha yake, katika kipindi hiki cha uchungu ni kipindi 

kinachohitaji, mahusiano mazuri kati ya mamamjamzito na mtoa 

huduma wa afya, mawasiliano mazuri na ushirikiano wa kutosha 

kati ya hawa watu ni vitu muhimu katika kipindi hiki cha uchungu, 

mama mjamzito anatakiwa awe mwerevu, msikivu na anaetoa 

ushirikiano wa kutosha kwa mtoa huduma ya afya anayemsaidia 

katika kipindi cha uchungu.

Hivyo bhasi ili kipindi hiki kigumu kiweze kuwa chepesi na cha 

kusaidika mamamjamzito hana budi kufanya au kuzingatia vitu 

vifuatavyo katika kipindi cha uchungu ili mambo yaweze kuwa 

mepesi

·       1. Kufanya mazoezi kama vile kutembea, kwenda na uchungu chini ( uchungu ukija chuchumaa chini)


·       2. Kunywa chai ya moto yenye sukari nyingi kwa ajili ya nguvu.
·       Kula vitafunwa kama vipo

·       3. Kuhema(kutoa hewa nje) kila uchungu unapokuja

·       4. Kusikiliza unachoambiwa na kuelekezwa na mkunga/daktari

·       5. Si  kila mama mjamzito anapopata uchungu unatakiwa asukume, anatakiwa asubiri mpaka pale atakapopewa amri ya kusukuma

·       6. Kutokubana miguu wakati wa kusukuma

·       7. Kutokusukuma kabla hajapewa amri ya kusukuma, mama mjamzito anatakiwa asukume pale tu anapoambiwa asukume

·       8. Wakati  wa kusukuma, mama mjamzito hatakiwi kuachia pumzi katikati ya msukumo

·       9. Na anapoambiwa kusukuma anatakiwa kusukuma kwa nguvu zote

·       9. Mama mjamzito anatakiwa Kuwa msikivu na mwerevu wakati wa uchungu pia toa ushirikiano kwa mkunga.

Hivi vitu vikifanyika na kuzingatiwa wakati wa  uchungu basi 

kipindi hiki cha uchungu kinaweza kutuletea matokeo mazuri ya 

ujauzito na matokeo mazuri ya ujauzito ni yale yanayo ambatana na 

kujifungua salama kwa afya ya mama na mtoto pia bila kuwa na 

matatizo yoyote.

IMEANDALIWA NA BARAKA EDGAR MLALO

REFERENCES

D.C.DUTTA, (2011) Text book of obstetrics, seventh edition, new central book agency (P) ltd, LONDON

GORDON W.GARLAND and ROSEMARY C. PERKES, (1959) a text book for pupil midwives, The English universities press ltd, LONDON.

LINDA K. BROWN and V.RUTH BENNETH, (1999) Myles textbook for midwives, thirteenth edition, Churchill Livingstone, EDINBURGH LONDON

1 comment:

Theme images by compassandcamera. Powered by Blogger.