DALILI HATARISHI KWA AFYA YA MTOTO MCHANGA.
Mtoto mchanga ni nani?
Mtoto mchanga ni mtoto mwenye umri wa siku 28 baada ya
kuzaliwa, afya ya mtoto mchanga huzidi kuimalika kadri
anavyozidi kukuwa.
mtoto mchanga anapokuwa na tatizo lolote la ki-afya au
anapokuwa anaumwa, ni vigumu kwa mzazi au mlezi
kufahamu kwasababu mtoto hawezi ongea anachohisi mwilini
mbali huyu mtoto ataonyesha ishara au dalili zinazoashilia
kuwa kuna kitu mwilini kinamsumbua na angependa
kupatiwa msaada.
hivyo basi ni jukumu la mzazi au mlezi kuweza kuzifahamu
hizo dalili ili aweze kuzitambua kipindi pale mtoto
atakapozionyesha, hizi ni baadhi ya hatarishi ambazo
zikionekana kwa mtoto basi huashiria kuwa mtoto anaumwa
au anashida na angependa kupewa huduma ya afya.
- kutokuwa na hamu ya chakula au kukataa kula chakula
- mwili wake kupata joto kali
- kupata dege dege
- kupoteza fahamu
- kupumua kwa haraka/kupumua kwa shida
- kutohisi kitu chochote, mfano akishituliwa
- kutoa sauti akiwa ana pumua
- kuwa wa baridi sana
- mwili wake kuwa wa njano
- kutopata choo ndani ya masaa 24
- kulia bila sababu inayoweza kujulikana
- uso wake kuwa wa bluu
No comments