MAAMBUKIZI YA CORONA VIRUSI KWA MAMA-MJAMZITO
Mwanamke akipata ujauzito kinga yake ya mwili hubadilika na
kuwa chini hivyo kumuweka katika hatari ya kupata magonjwa
mbalimbali katika kipindi cha ujauzito, wanasayansi wanasema
kuwa mabadiliko ya kinga ya mwili yanayotokea katika kipindi
cha ujauzito yanamuweka mama-mjamzito katika hatari kubwa
ya kupata maambukizi ya virusi vya corona kuliko mama asiye
mjamzito, pia mama- mjamzito yupo mwenye maambukizi ya
virusi vya corona yupo katika hatari ya kujifungua kabla ya umri
wa mimba wa kujifungua.
Wanasayansi wanaendelea kuchunguza kwa kina kirusi cha
corona na madhara yake kwa ujauzito, lakini kwa sasa ni vyema
mama-mjamzito akachukua tahadhari ya kujikinga na
maambukizi ya virusi vya corona kwa
- · kunawa mikono na sabuni/sanitizer
- · kuvaa barakoa usoni kwa kufunika mdomo na pua
- · kujiepusha na misongamano ya watu wengi
IIIIMETAFISIRIWA NA BARAKA EDGAR MLALO, AFISA MKUNGA, KUTOKA KWENYE TOVUTI YA www.cdc.gov
No comments