MAANDALIZI KABLA YA KUJIFUNGUA UJAUZITO/UCHUNGU
- Maandalizi kabla ya kujifungua au uchungu ni suala la muhimu linalotakiwa lihusishe familia, ndugu na jamaa kwaajiri ya kupata ushirikiano wa kutosha kwenye kipindi cha uchungu. Ni muhimu kufanya maandalizi kabla ya kujifungua, hii humsaidia mama mjamzito kuanda na kujua vitu vyote muhimu vinavyohitajika wakati wa kujifungua kwani uchungu huanza wakati wowote na mahali popote, pia uchungu huwa hautoi taarifa siku gani utaanza.
- Muda muafaka wa kunza kufanya maandalizi ya kujifungua ni kuanzia siku mama-mjamzito anapoanza kliniki ya mama-mjazito, ujauzito ukifikia wiki 37 ambazo ni sawa na miezi tisa na wiki moja, mama-mjamzito anatakiwa awe ameshakamilisha maandalizi haya na kujua taarifa muhimu zinazohusu ujauzito wake.
- Vitu muhimu vya kujua katika maandalizi kabla ya kujifungua au uchungu ni kama vile:
- Taarifa zinazohusu ujauzito.
- Siku ya makadilio; ni tarehe ambayo mama mjamzito alikadiliwa kujifungua au uchungu utaanza, siku hii ni muhimu mama mjamzito kuifahamu, si yeye tu bali hata mme, mwenza hata ndugu wanatakiwa kuifahamu. Japokuwa si lazima mama mjamzito kujifungua au uchungu kuanza tarehe husika, lakini ni muhimu kuifahamu kwani husaidia kujua kama umri wa mimba umepitiliza au uchungu umeanza kabla ya muda wake.
- Umri wa mimba; mama mjamzito anatakiwa kufahamu umri wa ujauzito wake kwa wiki au miezi toka alipojua kuwa yeye ni mjamzito, hizi taarifa huzipata akiwa anahudhuria kliniki, hivyo ni jukumu lake kujua umri wa ujauzito wake kila siku.
- Njia sahihi ya kujifungua; mama mjamzito anatakiwa kujua kama atajifungua kwa kawaida au upasuaji kabla ya uchungu, anatakiwa aelezwe njia ipi itamfaa wakati wa kujifungua kutokana na hali yake ya afya aliyopo nayo, taarifa hizi anatakiwa kuzipata kliniki kutoka kwa daktari au mkunga. Japokuwa si lazima njia aliyoambiwa ndiyo hiyo itakayotumika, mambo hubadilika wakati wa uchungu, lakini ni muhimu kujua kabla hajaanza uchungu.
- Sehemu ya kujifungulia; mama mjamzito kutokana na afya yake anatakiwa kujua sehemu ipi inayotoa huduma za afya anatakiwa kujifungulia, kati ya zahanati, kituo cha afya, hospitali ya wilaya, mkoa au rufaa, pia ni chaguo lake mwenyewe, ila anatakiwa kuchagua sehemu ambayo itaweza kutoa huduma sitahiki kutokana na afya yake na ujauzito pia.
2. Mambo yanayohusu uchungu.
- Huduma ya msaada (supportive care); mama mjamzito na familia wanahusika kwa hili, familia au mama majamzito lazima iandae mtu wa kumsaidia au kuwa nae wakati wa uchungu hospitali, huyu mtu ni muhimu wakati wa kuchangia taarifa na maamuzi, anaweza kuwa mme, mwenza, ndugu au hata rafiki. Pia mtu atakaye baki na watoto nyumbani.
- Maandalizi ya kifedha; mama mjamzito au familia wanatakiwa kujiandaa kiuchumi toka mimba ilipogundulika, bajeti ya kujifungua inatakiwa kuwa imeshaandaliwa. Japokuwa huduma ya kujifungua katika hospitali za serikali ni bure, lakini ni muhmu kufanya maandalizi ya kifedha kwa ajili ya mambo mengine ambayo yanaweza jitokeza katika kipindi cha kujifungua.
- Usafiri; mama mjamzto au familia yake wanatakiwa kuandaa njia ya usafiri itakayotumika kumpeleka mama mjamzito katika kituo cha afya pia kumrudisha nyumbani baada ya kujifungua. Ni vyema mama majamzito akapata njia ya usafiri ya kuaminika na yenye usalama kwake na mtoto wake.
- Nguo; mama mjamzito anatakiwa aandae nguo kwaajiri yake na mtoto wake, nguo zinazohitajika ni nguo za maternity kama vile dela, khanga, vitenge, babyshow ya mtoto, kofia, soksi na nguo za vichanga, pia anatakiwa aandae pamba, sanitary peds, pamps, whipers, gloves na vitu vitakavyotumika wakati wa kujifungua. Hivi vitu vyote vinatakiwa viwekwe kwenye bag moja atakalo enda nalo hospitali.
- Chakula; mama mjamzito anaruhusiwa kula kipindi cha uchungu, hivyo basi chakula ni muhimu sana katika kipindi cha kujifungua, mama mjamzito au familia inatakiwa kuandaa chakula na kuwepo muda wote wa uchungu, aina ya chakula chochote kinaruhusiwa lakini ni muhimu kuandaa vyakula ambavyo ni vyepesi kulika kuupa mwili nguvu katika hali ya uchungu, vyakula kama vile, chai, uji, mtori, cake, tende na maji ya kunywa.
- Uchangiaji wa damu; mama mjamzito katika kipindi cha kujifungua yupo katika hatari ya kupoteza damu nyingi hali ambayo inaweza kumfanya akapoteza uhai wake, japokuwa si lazima lakini ni muhimu kuandaa mtu husika takayejitolea kuchagia damu endapo tu itahitajika, huyu mtu anatakiwa aendane aina ya kundi la damu na mama mjamzito.




No comments