MADHARA YA MATUMIZI YA P2
Vidonge vya dharura ya uzazi wa mpango au P2 havina madhara
kwa mtumiaji endapo tu vitatumika ipasavyo. matumizi ya P2
yanatakiwa yatumike pale tu dharura inapotokea, P2 haitakiwi
kutumika kama njia ya uzazi wa mpango, bali inatakiwa itumike
kama njia ya dharura ya uzazi wa mpango.
ni vyema kutumia njia zingine za uzazi wa mpango kama una lengo
la kutopata ujauzito na sio kutengemea P2. njia hizi za uzazi wa
mpango ni kama vile sindano, vidonge, kitanzi, jiti na condom.
matumizi holela ya P2 huweza ambatana na mvurugiko wa
mzunguko wa hedhi (hormone imbalance) hivyo kuleta usumbufu
katika upatikanaji wa mimba kwa wakati itakapohitajika. pia
matumizi holela ya P2 humuweka mteja katika hatari ya kupata
maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile UKIMWI,
KASENDWE NA KISONONO.
pia matumizi ya P2 huambatana na maudhi kama vile vichomi,
kichefuchefu, matone ya damu, matiti kujaa, kutapika, uchovu wa
mwili, mvurugiko wa mzunguko wa hedhi, maumivu ya tumbo,
maumivu ya kichwa. hizi dalili ni za kawaida na si madhara kwa
mtumiaji wa P2 na hupotea zenyewe bila matumizi ya dawa.
matumizi sahihi ya P2 humsaidia mtumiaji asipate mimba na asipate
madhara yoyote yanayosababishwa na P2, hivyo unashauliwa
kutumia P2 wakati wa dharura tu na sio kila utakapofanya tendo la
ndoa,
No comments