KIFAFA CHA MIMBA

  • Ni hali ambayo huweza kumtokea mama-mjamzito, wenye umri wa miezi mitano sawa na wiki 20, mwenye msukumo wa damu mkubwa wa kuanzia 140/90mmHg na zaidi, ambapo mama-mjamzito mwenye huu msukumo wa damu huanguka kifafa mara moja au zaidi, hii hali hutokea kipindi cha ujauzito au ndani ya siku 42 baada ya kujifungua.

                                        

  • Hali hii ya kupata kifafa kipindi cha ujauzito husababishwa na msukumo wa damu kuwa mkubwa ambao haujatibiwa na kama hautagundulika mapema na kuachwa kutibiwa husababisha mama mjamzito kupata kifafa na kama hatua za kumtibu hazitachukulika husababisha kifo kwa mtoto na mama pia.
  • Lakini si kila mama-mjamzito mwenye msukumo wa damu mkubwa (pressure) anaweza kupata kifafa cha mimba, ila hali hii humuweka mama mjamzito katika hatari ya kupata kifafa cha mimba kama hatogundulika na kupewa huduma mapema.

  • Hivyo basi ni vyema kufanya uchunguzi mapema kuhusu afya ya mama mjamzito ili kuweza kuelewa kama msukumo wa damu ni mkubwa na kama unahitaji matibabu na kwa wale wanawake wanaojifahamu kuwa wana shinikizo la damu ni vyema kuonana na watoa huduma za afya ili kuweza kuchukua hatua sitahiki za kujilinda na kifafa cha mimba. Hivyo basi uhudhuriaji wa kliniki ya wajawazito ni muhimu sana.

WASILIANA NASI KWA UFAHAMU ZAIDI +255757599024-what's app.

No comments

Theme images by compassandcamera. Powered by Blogger.