AINA YA VYAKULA AU VIRUTUBISHO VILIVYO KWENYE MAZIWA YA MAMA.
- Maziwa ya mama yana kila aina ya virutubisho vinavyohitajika katika afya ya mtoto mchanga na ukuaji wake, virutubisho hivi vipo katika kiwango sitahiki kutokana na mahitaji ya mtoto. Ubora wa maziwa ya mama huchangiwa kwa kuwa na kila aina ya vyakula au virutubisho muhimu kwa mtoto pia kuwepo na kinga za mwili ambazo humsaidia kumlinda mtoto na magonjwa mbalimbali.
- Maziwa ya mama yana kiasi sitahiki ya virutubisho vinavyohitajika kwa kila mlo wa mtoto, hivyo kutohitaji mbadala wa chakula, pia maziwa ya mama hayahitajiki kuchemshwa, joto la mwili la mama linatosha kabisa kwa matumizi ya mtoto. Wingi wa virutubisho kwenye maziwa ya mama hutegemea na chakula na lishe mbadala kipindi cha ujauzito na unyonyeshaji, hivyo basi mama mjamzito hana budi kuzingatia mlo kamili katika vipindi hivyo, hivi ni baadhi ya virutubisho au aina ya vyakula vinavyopatikana kwenye maziwa ya mama.
- Protein; maziwa ya mama yana protein aina mbili whey na casein, virutubisho hivi ni muhimu kwenye afya ya mtoto kwani husaidia kwenye ukuaji na maendeleo ya mtoto, huimarisha kinga ya mwili ya mtoto, na kuchochea upatikanaji wa virutubisho vingine kama vile madini. Pia protein iliyopo kwenye maziwa ya mama ni bora kutokana na urahisi wake wakati wa mmeng'enyo, kuliko iliyopo kwenye maziwa ya kopo.
- Mafuta; maziwa ya mama yana mafuta ambayo ni muhimu kwa afya ya mtoto, mafuta yaliyoko kwenye maziwa ya mama husaidia mtoto katika ukuaji na maendeleo ya mfumo wa fahamu hasa ubongo, upatikanaji wa vitamini mwilini, na kama chanzo cha nishati mwilini.
- Vitaminis; maziwa ya mama yana kila aina ya vitamini muhimu katika mwili wa binadamu, ambazo hizi vitamini humkinga mtoto na maradhi mbalimbali. Mfano wa vitamini zilizopo kwenye maziwa ya mama ni kama vile, vitamini A, D, E, K, C na aina za vitamini B.
- Wanga; maziwa ya mama yana wanga aina ya lactose, ambayo ni wanga ipatikanayo kwenye maziwa tu. Aina hii ya chakula humsaidia mtoto kupata nguvu pia kulinda mwili na maradhi. Wingi wa wanga kwenye maziwa ya mama hutegemea na chakula anachokula mama wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua.
- Madini; maziwa ya mama yana madini, ambayo husaidia katika ukuaji na maendeleo ya mtoto, upatikanaji wa madini haya kwenye maziwa ya mama hutegemea vyakula na matumizi ya lishe mbadala. Mfano wa madini yapatikanayo kwenye maziwa ya mama ni kama vile, calcium, phosphorus, sodium, potassium, magnesium, bila kusahau iron, zinc, copper, manganese, na selenium.
- Maji; sehemu kubwa ya maziwa ya mama imetengenezwa na maji ambayo humsaidia mtoto kukata kiu pia kuondoa uchafu mwilini, maji yaliyoko kwenye maziwa ya mama ni mengi na yanatosha kwa mahitaji ya mtoto, hivyo basi mtoto kwa muda wa miezi sita ya mwanzo haitaji maji kutoka sehemu nyingine zaidi yaliyoko kwenye maziwa.
FAIDA ZA MAZIWA YA MAMA KWA MTOTO.
- Kinga; maziwa ya mama yana kinga za mwili hivyo humlinda mtoto asipatwe na maambukizi ya magonjwa mbalimbali.
- Virutubisho vingi; maziwa ya mama yana virutubisho mbalimbali vilivyo katika viwango sitahiki kwa ajiri ya afya na ukuaji wa mtoto, hivyo kumukinga mtoto asipate unene uliopililiza.
- Asili; maziwa ya mama ni asili hayajatengenezwa na kemikali za viwandani hivyo humsaidia mtoto asipate mzio (allergy).
- Hayana gharama; maziwa ya mama si ghari na upatikanaji wake ni wa haraka zaidi.
- Mepesi kulika; maziwa ya mama ni mepesi kumeng'enywa, hivyo humkinga mtoto na choo kigumu na mchafuko wa tumbo.
- Safi na salama; maziwa ya mama ni safi na salama, hayana uchafu na hayahitaji kuchemshwa au kuchujwa
- Uwezo wa akili; maziwa ya mama humuongezea mtoto uwezo wa kufikiri.
No comments