UVIMBE KWENYE MFUKO WA UZAZI.

  • Ni uvimbe unaotokea ndani au nje ya mfuko wa uzazi wa mwanamke, ambapo sababu yake kuu haijajulikana lakini wataalamu wa magonjwa ya kina mama wanasema hutokea kwasababu ya ongezeko la homoni ya estrogen mwilini mwa mwanamke. Mara nyingi uvimbe hutokea katika umri wa uzazi wa mwanamke (15-49), na hukua kwa haraka kipindi cha ujauzito na kwa wanawake wanaotumia vidonge vya uzazi wa mpango.

AINA ZA UVIMBE KWENYE MFUKO WA UZAZI.
    1. Uvimbe nje ya kizazi.
    2. Uvimbe kwenye misuli ya kizazi.
    3. Uvimbe ndani ya kizazi.

SABABU HATARISHI ZA KUPATA UVIMBE KWENYE MFUKO WA UZAZI.

    • Ujauzito.
    • Historia ya familia kupata uvimbe.
    • Mwanamke mwenye umri zaidi ya miaka 30.
    • Mwanamke mwenye uzito mkubwa.
    • Mwanamke aliyeko kwenye umri wa uzazi (15-49).
    • Mwanamke aliyewahi kuvunja ungo mapema chini ya miaka 12.
    • Mwanamke anayetumia vidonge ya uzazi wa mpango.
    • Mwanamke mwenye upungufu wa vitamin D.
    • Mwanamke mwenye tabia ya kula nyama nyekundu kwa wingi.
    • Mwanamke anayetumia pombe.

DALILI ZA UVIMBE KWENYE MFUKO WA UZAZI.

    • Kutokwa na damu nyingi za hedhi kwa muda mrefu.
    • Kutokwa na damu katikati ya mzunguko wa hedhi.
    • Kuhisi uzito na maumivu kwenye nyonga.
    • Maumivu nyuma ya miguu
    • Tumbo kuwa kubwa na kuhisi limejaa
    • Kupata maumivu ya mgongo.
    • Kupata maumivu wakati wa kujamiana.
    • Kuhisi kibofu kizito na kupata haja ndogo mara kwa mara.
MADHARA YA UVIMBE KWENYE MFUKO WA UZAZI.
    • Husababisha ugumba.
    • Husababisha uharibikaji wa mimba.
    • Husababisha uchungu kuanza mapema kabla ya siku ya makadilio kwa wale wenye mimba.
    • Hupunguza wingi wa damu mwilini.

WASILIANA NASI KWA UFAHAMU ZAIDI +255757599024-what's app.

No comments

Theme images by compassandcamera. Powered by Blogger.