MADHARA YA UTOAJI MIMBA.

  • Utoaji mimba sio kitu sahihi na kizuri kwenye mwili wa mwanamke, huduma hii huambatana na maudhi pia madhara mengi ambayo yasipoweza tambulika na kutibiwa mapema huweza sababisha maafa. Matatizo yanayoambatana na utoaji mimba hutokea kwa kutegemea na njia iliyotumika kutoa mimba,  uzoefu hafifu wa mtoaji, vifaa na mazingira yaliyotumika katika hatua za kutoa mimba. Madhara au matatizo ambayo huambatana na utoaji mimba ni kama vile;

    • Maambukizi ya magonjwa; utoaji wa mimba huambatana na magonjwa kama vile PID au bacteria vaginosis. Maambukizi haya katika mfumo wa uzazi huweza sababisha ugumba kama yatakaa kwa muda mrefu bila kutibiwa. Mtoaji wa mimba anatakiwa apate huduma baada ya utoaji mimba ili kuzuia uwezekano wa kupata maambukizi haya.
    • Uharibifu wa tumbo la uzazi; utoaji wa mimba hasa kwa njia ya vifaa huweza sababisha kwa bahati mbaya kutobolewa au kukwanguliwa zaidi, hivyo kusababisha mtolewaji kupata vitu viwili aidha maambukizi au kuvuja kwa damu nyingi na kupoteza maisha.
    • Kubaki kwa baadhi ya masalia ya uzazi; hii hutokea baada ya kutoa mimba lakini kwa bahati mbaya baadhi ya mabaki ya uzazi yakabaki ndani ya mfuko wa uzazi na kupelekea mtolewaji wa mimba kuendelea kutokwa na damu mfurulizo, pia hata kupata maambukizi.
    • Kutokwa na damu nyingi; utoaji wa mimba hasa kwa njia ya vidonge huambatana na utokwaji wa damu nyingi kwa mtolewaji, hali hii huweza msababishia mauti kama haitapatiwa ufumbuzi au huduma mapema.
    • Kifo; pia utoaji mimba huweza sababisha kifo cha papo kwa papo.
    • Mimba iliyotungwa nje ya kizazi; utoaji mimba pia huweza sababisha mimba kutungwa nje ya mfuko wa uzazi.
    • Ugumba; utoaji mimba hasa kwa njia ya vifaa huweza sababisha ugumba. 
    • Kulegea kwa shingo ya uzazi; utoaji wa mimba mara kwa mara kwa njia ya vifaa husababisha shingo ya uzazi kupoteza ustahimirifu wake na kulegea, hali hii husababisha utokaji wa mimba mara kwa mara.
    • Saratani ya matiti; mwanamke anayetoa mimba mara kwa mara yupo kwenye hatari ya kupata saratani ya matiti.
  • Utumiaji wa njia za kisasa za uzazi wa mpango huepusha utungwaji wa mimba zisizotarajiwa au kupangwa, hivyo basi kuepusha kabisa maamuzi ya kutoa mimba.

No comments

Theme images by compassandcamera. Powered by Blogger.