UMUHIMU WA FOLIC ACID KWA MAMA-MJAMZITO.
- Folic acid ni vitamini iliopo katika kundi la vitamin B, vitamini hizi kazi zake husaidia mfumo wa fahamu katika ufanisi wake wa kazi, pia husaidia mwili kutengeneza nguvu kutoka kwenye vyakula mbalimbali tunavyokula.
- Mwili wa binadamu hauna uwezo wakutengenezi folic acid, hivyo basi binadamu hutegemea folic acid kutoka kwenye vyakula mbalimbali ambavyo vina wingi wa vitamini hii. Folic acid (vitamini B9) inayopatikana kwenye vyakula huitwa folate na ile inayotengenezwa na kuwekwa kwenye vyakula kama vile mikate, unga au mchele huitwa folic acid. Folate hupatikana kwa wingi kwenye mbogamboga, nyama, maziwa, maharage, mayai, matunda na maini.
- Folic acid au vitamini B9, ni muhimu katika hatua ya uumbaji na maendeleo ya mtoto akiwa tumboni (kijusi), vitamini hii hutumika katika utengenezaji wa seli za mwili pamoja na DNA ambazo huhusika katika kutoa taarifa za uumbaji wa viungo mwilini. Hivyo basi upungufu wa vitamini hii mwilini wa binadamu hupelekea upungufu wa cell na DNA mpya, kwa mama mjamzito upungufu wa vitamini B9 au folic acid husababisha baadhi ya viungo vya mtoto visiumbwe na kusababisha mtoto kuzaliwa akiwa hana baadhi ya viungo vya mwili.
- Mama-mjamzito anauwezekano mkubwa wa kujifungua mtoto mwenye tatizo la mfumo wa fahamu kama vile mgongo wazi kama asipokuwa na folic acid za kutosha mwilini kabla ya ujauzito na hakuweza kupata lishe mbadala ya folic acid katika kipindi cha ujauzito. Hivyo basi ni muhimu kwa mwanamke aliyepo kwenye umri wa uzazi kumeza vidonge vya folic acid kama lishe mbadala ili kuepusha watoto kuzaliwa wakiwa na mgongo wazi.
- Mama-mjamzito anatakiwa aanze mapema kutumia vidonge vya folic acid mara tu anapogundua ni mjamzito, tena inashauriwa matumizi ya folic acid kabla ya kushika ujauzito ndo husaidia mtoto kutopata mgongo wazi. Mama-mjamzito akichelewa kutumia vidonge vya folic acid kuna uwezekano mkubwa kujifungua mtoto aliye na kasoro kwenye mfumo wa famu kama vile mgongo wazi. Hivyo basi ni muhimu na kuzingatia utumiaji wa folic acid kabla ya kushika ujauzito.
NANI ANATAKIWA KUTUMIA FOLIC ACID.
- Mwanamke yeyote yule aliyeko katika umri wa uzazi (15-49).
- mwanamke anayepanga kushika ujauzito.
- mwanamke mlevi wa pombe anae kunywa zaidi ya chupa mbili za bia kwa siku, anatakiwa atumie folic acid mwezi mmoja kabla hajashika ujauzito na kuacha kabisa utumiaji wa pombe.
- mwanamke aliyopo kwenye matumizi ya vidonge vya kuzuia kifafa.
- mwanamke mwenye ujauzito.
- mwanamke anayenyonyesha.
No comments