DALILI ZA UJAUZITO


  • Mwanamke akipata ujauzito mwili wake hupatwa na mabadiliko ambayo haya mabadiliko huweza tumika kama dalili za ujauzito japokuwa sio kila hayo mabadiliko huashilia kuwa mwanamke ni mjamzito, hivyo basi mwanamke akishaona baadhi ya mabadiliko hana budi kupima uwepo wa ujauzito ili aweze kuthibitisha kama kweli ni mjamzito.
                                                                         
  • Hizi ni baadhi ya dalili za mapema ambazo huweza mtokea mwanamke hivyo kumpa wasiwasi kama ni mjamzito. 
  1. Kutopata hedhi(damu) ya mwisho wa mwezi
  2. Matiti kujaa au kuvimba
  3. Matiti kutoa maji maji(maziwa)
  4. Kichefuchefu
  5. Kuchoka kwa mwili
  6. Kupatwa na ongezeko la haja ndogo
  7. Uso kutokwa na chunusi
  8. Kukosa na hamu ya kula
  9. Kuchukia baadhi ya vyakula
  10. Ongezeko la maji maji ya ukeni
  • Si lazima mwanamke akipatwa na baadhi ya hizo dalili hapo juu basi zinamaanisha  tayari ameshapata ujauzito, lakini mwanamke kipata baadhi ya hizo dalili na akawa hajapata damu zake za mwisho wa mwezi basi hana budi kupima kipimo cha mimba na kuthibitisha uwepo wa ujauzito
WASILIANA NASI KWA UFAHAMU ZAIDI +255757599024-what's app.                                                
i

No comments

Theme images by compassandcamera. Powered by Blogger.