Ni blog inayohusu mambo ya afya ya uzazi, katika blog hii utaweza pata ufahamu na kuelimika kuhusu mambo mbalimbali yanayo husu afya ya uzazi na mahusiano.
A blog page concerned with the provision of health information related to sexual and reproductive health.
Mimba ni hali ya kubeba kijusi/vijusi vinavyokuwa na kuendelea tumboni mwa mwanamke. Mimba hutokea au hupatikana pale tu yai la kike
na mbegu ya mwanaume kukutana na kutengeneza kijusi ambacho hukaa kwenye tumbo
la uzazi mpaka pale kitakapotolewa nje ya tumbo la uzazi kama mtoto mchanga,
katika kipindi hiki mwanamke hapati damu zake za mwezi kwa muda wa takribani
wiki 40 sawa na siku 280.
Mwanamke alie na mimba huitwa
mama mjamzito au mjamzito, katika kipindi hiki mama mjamzito hupata mabadiliko
ya kimwili na kiakili pia, ambayo hujizihilisha kama dalili za ujauzito.
Ujauzito umegawanyika katika
vipindi vitatu, kipindi cha kwanza kinachoanza wiki 0-12, kipindi cha pili
wiki13-28 na kipindi cha tatu wiki 29 hadi kujifungua.
Katika kila vipindi vya ujauzito kuna mabadiliko ambayo hutokea kwenye kila
kipindi ambayo hayo mabadiliko hutumika kama dalili za ujauzito.
WASILIANA NASI KWA UFAHAMU ZAIDI +255757599024-what's app.
No comments