DALILI ZA KIFAFA CHA MIMBA
Kwa mama-mjamzito ni vyema kuzifahamu dalili za kifafa cha
mimba ili aweze kuchukua hatua za ki-afya pale tu anapohisi hizi
dalili, kwani kifafa cha mimba kinatibika na kinadhuirika kama
mama-mjamzito mwenye hizi dalili atagundulika mapema. zifuatazo
ni dalili za kifafa cha mimba.
- msukumo wa damu kuwa sawa au zaidi ya 140/90mmHg
- maumivu ya kichwa hasa kipanda uso
- kuona maluweluwe
- kupata maumivu ya tumbo la juu
- mkojo kuwa na kiasi kingi cha protein
- kuvimba mwili mzima
- kutopata mkojo au kupata mkojo kiasi
- kuongezeka uzito
- kichefuchefu kilichozidi na kutapika sana
hizo ni viashiria vya kifafa cha mimba, kiashiria kikuu ni shimikizo
la damu kuwa sawa au zaidi ya 140/90mmHg kwa mama-mjamzito.
No comments