KIFAFA CHA MIMBA
Ni hali ambayo huweza kumtokea mama-mjamzito wenye
umri wa miezi mitano sawa na wiki 20, mwenye msukumo wa
damu mkubwa wa kuanzia 140/90mmHg na zaidi, ambapo
mama-mjamzito mwenye huu msukumo wa damu huanguka
kifafa mara moja au zaidi, hii hali hutokea kipindi cha ujauzito
au ndani ya siku 42 baada ya kujifungua.
hali hii ya kupata kifafa kipindi cha ujauzito husababishwa na
msukumo wa damu kuwa mkubwa ambao haujatibiwa na
kama hautagundulika mapema na kuachwa kutibiwa
husababisha mama mjamzito kupata kifafa na kama hatua za
kumtibu hazitachukulika husababisha kifo kwa mtoto na
mama pia.
lakini si kila mama-mjamzito mwenye msukumo wa damu
mkubwa (pressure) anaweza kupata kifafa cha mimba, ila hali
hii humuweka mama mjamzito katika hatari ya kupata kifafa
cha mimba kama hatogundulika na kupewa huduma mapema.
hivyo basi ni vyema kufanya uchunguzi mapema kuhusu afya
ya mama mjamzito ili kuweza kuelewa kama msukumo wa
damu ni mkubwa na kama unahitaji matibabu na kwa wale
wanawake wanaojifahamu kuwa wana shinikizo la damu ni
vyema kuonana na watoa huduma za afya ili kuweza kuchukua
hatua sitahiki za kujilinda na kifafa cha mimba.
Hivyo basi uhudhuriaji wa kliniki ya wajawazito ni muhimu sana
IMEANDALIWA NA BARAKA EDGAR MLALO, AFISA MKUNGA
No comments