UMUHIMU WA KUNYONYESHA MAZIWA YA MAMA
Maziwa ya mama yana kila aina ya virutubisho vinavyohitajika
katika afya ya mtoto mchanga na ukuaji wake, virutubisho hivi vipo
katika kiwango sitahiki kutokana na mahitaji ya mtoto. maziwa ya
mama yana umuhimu na faida nyingi sana katika afya ya mtoto na
ukuaji wake. zifuatazo ni faida za maziwa ya mama.
- maziwa ya mama yana kinga za mwili hivyo humlinda mtoto asipatwe na maambukizi ya magonjwa mbalimbali
- maziwa ya mama yana virutubisho mbalimbali vilivyo katika viwango sitahiki kwa ajiri ya afya na ukuaji wa mtoto, hivyo kumukinga mtoto asipate unene uliopililiza
- maziwa ya mama ni asili hayajatengenezwa na kemikali za viwandani hivyo humsaidia mtoto asipate miziro (allergy)
- maziwa ya mama si ghari na upatikanaji wake ni wa haraka zaidi
- maziwa ya mama ni mepesi kumeng'enywa, hivyo humkinga mtoto na choo kigumu na mchafuko wa tumbo
- maziwa ya mama ni safi na salama, hayana uchafu na hayahitaji kuchemshwa au kuchujwa
- maziwa ya mama humuongezea mtoto uwezo wa kufikiri
No comments