FAHAMU KUHUSU P2
P2- Ni njia ya uzazi wa mpango inayotumika katika hali ya dharura,
hivyo kuitwa njia ya dharura ya uzazi wa mpango. hufahamika pia
kama morning after pills, emergency contraceptives, plan B.
njia hii ya uzazi wa mpango huzuia mimba kutungwa na sio njia ya
kutoa mimba, hivyo matumizi yake yanatakiwa yatumike kipindi
cha dharura tu na sio kama njia ya kutoa mimba au njia za kawaida
za uzazi wa mpango.
P2 kama njia zingine za uzazi wa mpango zenye vichocheo
(hormone), inatumia vichocheo (hormone) kuzuia mimba
(implantation) na kuzuia uchwavushwaji wa yai (ovulation).
tofauti kati ya P2 na njia zingine za uzazi wa mpango ni kwamba P2
inatumika kwenye mazingira ya dharura wakati njia zingine za uzazi
wa mpango zinatumika kila siku au kila miezi na miaka ili kuzuia
mimba.
mazingira ya dharura ambayo P2 inaruhusiwa kutumika ni kama vile;
1. mwanamke aliyebakwa na hataki kushika ujauzito wa mbakaji
2. kupasuka au kuchomoka kwa condom na shahawa kuingia kwenye uke
3.kufanya tendo la ndoa katika siku za kushika mimba bila kutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango
4. mtumiaji wa vidonge vya uzazi wa mpango kusahau kumeza vidonge kwa siku tatu (3) mfululizo na akafanya tendo la ndoa.
P2 ikitumika mapema baada ya dharura kutokea huweza kuzuia mimba.
No comments