JINSI YA KUTUMIA P2 - MATUMIZI YA P2
Matumizi ya P2 hutegemea na aina ya njia ya dharura unayotumia,
kuna aina mbili zinazotumika kama njia za dharura za uzazi wa
mpango.
1. vidonge
2. kitanzi
vidonge ndo njia inayotumika sana kuliko kitanzi, hizi njia zote
ufanisi wake unapungua mara baada ya masaa 120 (siku 5) kupita
bila kutumika, maana yake njia za dharura za uzazi wa mpango
zinatakiwa kutumika ndani ya masaa 120 (siku 5) baada ya dharura
kutokea na ufanisi unaongezeka zaidi kama zitatumuka ndani ya
masaa 72 (siku3) baada ya dharura kutokea.
kitanzi hutakiwa kuwekwa ndani ya masaa 120 (siku 5) baada ya
dharura kutokea, utumiaji wa kitanzi baada ya masaa 120 (siku 5)
huambatana na kutozuia mimba, hivyo basi unashauriwa kutumia
njia hii ndani ya muda muafaka.
vidonge hutakiwa kutumika ndani ya masaa 120 (siku 5) baada ya
dharura kutokea, ufanisi wa utendaji kazi wake huongezeka zaidi
vinapotumiaka mapema baada ya dharura kutokea.
vidonge hivi hupatikana madukani vikiwa katika aina tofauti,
hupatikana kikiwa kidonge kimoja, ambacho humezwa mara moja.
vikiwa vidonge viwili, ambavyo humezwa mara mbili, kimoja baada
ya dharura na cha pili baada ya masaa kumi na mbili (12).
pia vidonge vya majira vya uzazi wa mpango vinaweza kutumika
kama njia ya dharura ya uzazi wa mpango, ambapo mtumiaji
anatakiwa kumeza jumla vidonge nane (8) ndani ya siku moja.
baada ya dharura anatakiwa kumeza vidonge vinne (4) na baada ya
masaa kumi na mbili (12) anamalizia vinne (4) vilivyobaki.
No comments